StopEpa.org
MAPATANO YA BIASHARA ZA EU-ACP ZIITWAZO ‘EPAs’ YAACHWE

Tangu mwaka wa 2002, Muungano wa Mataifa ya Uropa na mataifa ya Afrika, Carribean na vikundi vya Pacific ( ACP) wamekuwa wakishauriana juu ya kushirikiana kiuchumi (EPAs) kama sehemu ya Ushirika wa Cotonou. EPAs, imenuia kuanzisha mapatano ambayo yataondoa mazuio ya biashara kati ya EU na nchi za ACP” ambayo msingi wake ni “ kuunganisha nchi zilizoazishwa na ACP” na kuendeleza na kuhifadhi maendeleo na kusaidia kumaliza umaskini katika nchi za ACP”.

EPAs zilizoanzishwa wakati huu ni za kushauriana mapatano ya biashara kati ya nchi mbali mbali.

Mara kwa mara, EU {Muungano wa Uropa} imesisitiza kwamba EPAs iwe na msingi thabiti wa kufafanua amri za WTO na washughulikie kuondoa vikwazo vya biashara za EU-ACP asili mia tisini (90%), kwa muda mfupi iwezekanavyo. Zaidi ya hayo, EU inadai mazungumzo katika sehemu mbalimbali kama, kwenye nyanja za uwekezaji, mashindano, uanzilishaji wa biashara, uwakilishi wa serikali, ulindaji wa mambo ya hakika na huduma. Mashauri juu ya mambo hayo ya kwanza manne yalikataliwa na nchi za ACP katika WTO kwa sababu ya matokeo mabaya ya maendeleo. Kwa mpangilio mpya wa “ kushirikiana kiustawi” EU imeleta kiupya WTO uhuru wa biashara kupitia EPAs.

Hata ingawa chi za ACP zimeonyesha kutofurahia, Muungano wa Uropa umetilia mkazo kiuchumi na kiutawala kukimbilia mazungumzo ya biashara huru ya EPA bila matayarisho mema. Sauti kutoka Uropa na ACP zikiuhimiza Muungano kutafuta njia nyingine zilipuuzwa. Kwa sababu ya utegemeaji wa misaada ya nje, serikali za ACP hawana njia nyingine ila kukubaliana na matakwa ya EU, wakubalishe Uropa kuuza bidhaa soko zao. Mkazo huu wa utendawazi ulivyotiliwa nguvu katika mazungumzo ya EPA, wabainisha kwamba mapatano hayo ni ya kutanua kuingia kwa Uropa katika soko za ACP, badala ya kukuza nchi za ACP.

Nchi za ACP zimetilia maanani muungano wao kuleta maarifa na maendeleo. EPAs itahatarisha unyofu wa mawasiliano ya muungano na kuwachongea wafanyizaji wa ACP kwa ushindani usio halali katika soko za nchini na nje. Matokeo ni ukosefu mkubwa wa kazi, kupoteza uchumi, ukosefu wa chakula, na watu kutofautiana kiuchumi. Serikali za ACP zitaenda hasara sana kiuchumi, kwa kuondolewa fedha za bidhaa zinazoingia chini, na zitaendelea kutatizika na shida ya upotevu wa raslimali na ufadhili usioweza kurekebishwa. Ingawa Muungano wa Uropa waendelea, ubishi kuwa EPAs ni “ chombo cha maendeleo” kumechunguzwa na kuonekana kuwa mzigo wa kurekebisha EPAs utachukuliwa na nchi za ACP, pamoja na zile za LDCs.

EU imepunguza shabaha za Cotonou za kumaliza umaskini na kuhifadhi maendeleo na kuifanya biashara yao kujiendeleza binafsi na mpangilio wa kujikuza kiuchumi. EPAs itazidisha utawala na kutilia mkazo kampuni za Uropa, bidhaa na huduma. Kwa hivyo, EPAs itaongeza upana na urefu kupotoka kiuchumi na udhaifu wa siasa ambao unapatikana chi nyingi za ACP. Mapatano ya kibiashara ya EPAs ambayo ni ya nifanye nikufanye haisaidii kamwe nchi za ACP, kiuchumi wala kimaendeleo.

Kwa hivyo, twakataa kata kata huu “ mkatabu wa ushirikiano wa kiuchumi” kama unavyowaziwa sasa.

Tunataka kuchunguza na kukaguliwa kwa mpango mpya wenye busara wa biashara za nje za EU, mno kuhusu mataifa yanayohitaji kukua kiuchumi. Tunadai ushirikiano kibiashara kati ya EU-ACP yaimarishwe kwa msingi ufuatao:

  • Iwe na muundo wa kutotendeana mambo, kama ilivyo katika GSPs, na kusiwe na wengine wa maana zaidi katika WTO.
  • Masoko ya kinyumbani na ya eneo lote la wafanyizaji wa ACP yalindwe.
  • Ondoa mkazo wa biashara na uwekezaji wa utenda wazi.
  • Wakubali muda mwafaka wa kanuni na kuunga mkono nchi za ACP kuendeleza mikakati yao ya maendeleo.